Bariki Kenya lyrics

Songs   2025-01-10 03:51:19

Bariki Kenya lyrics

Mwenyezi Mungu napiga magoti

Nikiombea nchi yangu kenya

Amani upendo na umoja,

Kenya yetu amani tele

ufisadi ubinafsi ukabila,

adui zetu Kenya wanatutesa

vijana wetu umewamalika,

kweli shetani kaamulia Kenya

Ni wengi wametuacha, wengi wamelala salama

wengi wanateseka, ee Mungu ilinde Kenya

Baba kuwa unatupenda,

unatujali tena unatuwaza

Hawa wachafu wanachafua Kenya

Tumalizie daddy safisha Kenya

Shetani hauna uwezo,

kazi yako kuchanganya watu

kuharibu na kumaliza,

nakuamuru sasa uhame Kenya

Ni wengi wametuacha, wengi wamelala salama

wengi wanateseka, ee Mungu ilinde Kenya

Na tena narudisha shukrani

kwa viongozi Baba uliotupa

Kwa kuwa mi tena ni wakuheshimu,

Bariki kenya baba tufurahie

Roho wa Mungu, Bariki kenya

Daima kenya, amani tele

Kupingana hatuna, sote ni wakenya

Mliolala, laleni salama

Mwenyezi Mungu, Bariki Kenya

Ni wengi wametuacha,

wengi wamelala salama

wengi wanateseka,

ee Mungu ilinde Kenya

Na tena narudisha shukrani

kwa viongozi Baba uliotupa

Kwa kuwa mi tena ni wakuheshimu,

Bariki kenya baba tufurahie

Roho wa Mungu, Bariki kenya

amani tele, sote ni wakenya, laleni salama

Mwenyezi Mungu, Bariki Kenya

Swahili Worship Songs more
  • country:
  • Languages:Swahili, Chewa
  • Genre:
  • Official site:
  • Wiki:
Swahili Worship Songs Lyrics more
Excellent Songs recommendation
Popular Songs
Artists
Songs