Ex [Remix]

Songs   2024-12-23 13:13:57

Ex [Remix]

Kill it! Eeh...

Mimi Mars chuga queen

Ushanitoa nuksi

Kulalama lalama kisa penzi lanikoroga

We ndo mnganguzi

Ulionipa matibabu na ule utamu kunoga

Vidusi wavimbe kiukweli kweli

Vijuso vyao visio haya

Wivu wasonge wenye kejeli

Waficha nyeti kwa vijibwaya

Bendera yafuata upepo

Nilichotaka kishatimia

Tunasubiri kuiona pepo

Kwa vile Jah katutunukia

Ex nenda salama

Wasalimie hao vimada wa bomu wenye biti

Mwenzako nampa nyama

Haichomi anaileta kama ikiwa mbichi

Akinitomasa akinishika mpole mpole (mpole mpole)

Akinuna akicheka mpole mpole (mpole mpole)

Hebu mama usifanye hasira pole pole (pole pole)

Dunia inataka staara pole pole (pole pole)

[MwanaFa]

Nikikupigia nakucheki tu, sijamisi mikasibu

Miji ina mengi nauliza ka uko salama tu

Umenikosa najua ndo maana bado uko bitter

Na mpamba tulio naye ila bado unanikumbuka

Fujo za nini shida mbona? Si ajabu kushindwana

Vijembe moja kwa moja ka nimekuibia figo mama

Uvunguni so nishagoma kuinama

Nishakataa utumwa shika hamsini zako nenda

Usilete noma punguza mzuka

Fisi za Arusha zinapendaga kama vita

Ninapochana ndo utajuta utadhani ugomvi na Hitler

Battle la kimbio zako utazikumbuka

Nakuomba sana ka kuachana tuachane

Ka watu wazima, sio manoma utasema ndo watu wa kwanza kuachana

Au wa mwisho kupendana au ndo mfano wa kutemana

Sio milima sisi ni watu pengine tutakutana

Hebu mama usifanye hasira pole pole (pole pole)

Dunia inataka staara pole pole (pole pole)

Akinitomasa akinishika mpole mpole (mpole mpole)

Akinuna akicheka mpole mpole (mpole mpole)

I say, no no sitaki tena

In case you don't know

He is just like Maradona

Like Maradona...

Ex nenda salama

Wasalimie hao vimada wa bomu wenye biti

Mwenzako nampa nyama

Haichomi anaileta kama ikiwa mbichi

Akinitomasa akinishika mpole mpole (mpole mpole)

Akinuna akicheka mpole mpole (mpole mpole)

Akinitomasa akinishika mpole mpole (mpole mpole)

Akinuna akicheka mpole mpole (mpole mpole)

Mimi Mars more
  • country:Tanzania
  • Languages:Swahili
  • Genre:
  • Official site:
  • Wiki:
Mimi Mars Lyrics more
Excellent Songs recommendation
Popular Songs
Artists
Songs