Hauwezi Kushindana [You Cannot Compete] lyrics

Songs   2025-01-10 08:06:02

Hauwezi Kushindana [You Cannot Compete] lyrics

(REF)(2x)

Hauwezi kushindana, oh kushindana

Na mwanadamu mwenye kinywa

Kama maneno yangekuwa yanaweza kutoboa mwili huu

Mbona sasa ningekuwa na vidonda mwili mzima

Vita vya maneno kuna watu ni majemedari

Ukisema mshindane mbona mikono mtainua

Kupigwa vita ni kawaida isikusumbue

Wewe ni mti wenye matunda, zoea mawe

Lia kidogo, nyamaza ili uchungu uishe

Ukiendelea unawapa kichwa hao

Basi laza imani, rejea vitani

Wakikuona waseme, umekuwa sugu

Acha waongee, acha waseme seme

Ila yuko Mungu wakuwaziba midomo

(REF)

Ikiwa Mungu anahukumu kwa kusikiza maneno

Mbona hata matumbo ya mimba yanasemwa sana

Hivi Mungu angehukumu kwa kusikiza umbea

Si ningekushauri mchungaji wangu ufunge kanisa

Mwanadamu, mwanadamu shida ni ulimi

Ungejifunza ukimya, haunanga hasara

Fulani, we fulani una shida gani?

Na uongo wanini? Mwogope Mungu

Ukumbuke ni ahadi, kuna siku yaja

Kwa kila neno na kinywa chako utatolea hesabu

Mimi nimeshakwambia kubali uwache

Utajijua na shingo yako ngumu

Siwezi kushindana, oh kushindana

Na mwanadamu mwenye kinywa

(REF)

Yesu, huyu Yesu hakujitetea kabisa

Japo walimsema kwa ubaya aliwasamehe

Na wewe uwasamehe, uwaombee

Kwa maana hawayajui wasemaya

Wakifingyanga ubaya, uwajibu kwa wema

Usishindane na mtu, wajibu kwa wema

Ata iwe ni ndugu wa karibu, wajibu kwa wema

Si vizuri wewe, usilipe kisasi, wajibu kwa wema

Tena wema uende, wajibu kwa wema

Eh, wajibu kwa wema

Maana, Maana

Swahili Worship Songs more
  • country:
  • Languages:Swahili, Chewa
  • Genre:
  • Official site:
  • Wiki:
Swahili Worship Songs Lyrics more
Excellent Songs recommendation
Popular Songs
Artists
Songs