Mauzauza lyrics

Songs   2024-12-27 01:16:30

Mauzauza lyrics

Moko!

[Zuchu]

Shunu we usijipe mapana eti mwili kujitutumusha

Nitakutawanya, ka bahari na fimbo ya Musa

Umejigeuza soji

Si wa Korola wala Vogi

Na hilo wowowo la kufoji

Eti linakupa kodi

[Khadija Kopa]

Oooh leo unikome mwenye kiranga (mwenye kiranga)

Hujanijua vizuri hili timbwiri la vanga (mwenye kiranga)

Oooh leo mbona umeyabananga (mwenye kiranga)

Mi maskini jeuri sitegemei madanga (mwenye kiranga)

Mauzauza we mwana mauzauza

Si wamekushindwa kwenu walimwengu tutakufunza

Mauzauza we mwana mauzauza

Si wamekushindwa kwenu walimwengu tutakufunza

Una nini kichwa cha chikichi

Umevaa kinu unatwangia mchi

Hahaaa!

[Zuchu]

Mwali kigego mwenye nyota ya mitara

Hivi kungwi wako nani wewe? (atajijua)

Uso mitego imedoda biashara

Hueleweki si kunguru si mwewe

[Khadija Kopa]

Wa dala ubaki dala mwenzio mimi kibunja

Haufai kwa kafara si mbuzi wewe ni punda

[Zuchu]

Umejivesha ubazazi kwa mapana na marefu

Uso na kazi si wa ndala wala peku

[Khadija Kopa]

Ooooh

Hondo hondo mlezi wa wana

We budege zoazoa

Mwali pengo binti mwanya

Chuchunge kwa kudonyoa

Oooh leo unikome mwenye kiranga (mwenye kiranga)

Hujanijua vizuri hili timbwiri la vanga (mwenye kiranga)

Oooh leo mbona umeyabananga (mwenye kiranga)

Mi maskini jeuri sitegemei madanga (mwenye kiranga)

Mauzauza we mwana mauzauza

Si wamekushindwa kwenu walimwengu tutakufunza

Mauzauza we mwana mauzauza

Si wamekushindwa kwenu walimwengu tutakufunza

Hahaa kuvaa dira si kazi, kazi kulikamatia eeeh!

[Zuchu]

Utayaweza yangu, yako yanakushinda

Utayaweza yangu, yako yanakushinda

(oooh kisandobe)

Utayaweza yangu, yako yanakushinda

(uso kasi mwana wa kobe)

Utayaweza yangu, yako yanakushinda

(oooh unadidi dadi)

Utayaweza yangu, yako yanakushinda

(Usonoga kwa chumvi wala magadi)

Utayaweza yangu, yako yanakushinda

Hahaaaa

Mlezi wa wana bye!

  • Artist:Zuchu
  • Album:I Am Zuchu (2020)
Zuchu more
  • country:Tanzania
  • Languages:Swahili, English
  • Genre:
  • Official site:https://www.instagram.com/officialzuchu/
  • Wiki:https://en.wikipedia.org/wiki/Zuchu?wprov=sfti1
Zuchu Lyrics more
Zuchu Featuring Lyrics more
Excellent Songs recommendation
Popular Songs
Artists
Songs