Mwamba Wenye Imara lyrics
Songs
2025-01-10 07:28:20
Mwamba Wenye Imara lyrics
(2x)
Mwamba wenye imara,
Kwako nitajificha.
Maji na damu yako,
Toka mbavuni mwako,
Iwe dawa ya kosa,
Kutakasa mioyo.
(2x)
Si kazi za mikono,
Ziletazo wokovu.
Nikitoa machozi,
Nikifanya kwa bidii,
Siwezi kujiosha,
Unioshe wewe tu.
(2x)
Sina la mikononi,
Naja msalabani.
Ni uchi, nipe nguo,
Dhaifu, nipe nguvu,
Niondolee taka,
Nitakase sijafa.
(2x)
Nikaapo dunia,
Nifikapo kifoni.
Nitakapofufuka,
Nitakapokuona,
Mwamba wangu wa kale,
Kwako nitajificha.
- Artist:Swahili Worship Songs